MADRID, Hispania
LIONEL MESSI amempita Karim Benzema wa Real Madrid ambao ni mabingwa wa La Liga kwa idadi ya mabao manne.
Messi msimu wa 2019/20 ametupia mabao 25 na ametoa jumla ya pasi 21 zilizotengeneza mabao.
Benzema amefunga mabao 21 na kutoa jumla ya pasi nane za mabao ndani ya La Liga.
Messi amefunga jumla ya dakika 2,880 uwanjani akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 115.
Benzema amefunga jumla ya dakika 3,152 uwanjani akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 150.