NAIROBI,KENYA

VYOMBO  vya usalama mjini Mombasa vimemkamata Mansur Mohamed Surur, maarufu “Mansour”, raia wa Kenya na mtoro aliyekuwa akitafutwa na Marekani.

Surur inasemekana alikuwa anatafutwa na vyombo kadhaa vya usalama kwa kujihusisha nakusafirisha dawa za kulevya na biashara haramu ya pembe za ndovu na faru, ambao ni wanyama wanaoindwa na majangili, pembe hizo zina thamani ya dola milioni saba.

Uhalifu huo unaelezewa kuwa ulihusisha ujangili wa zaidi vifaru 35 na zaidi ya tembo 100.

Alikuwa kati ya raia 47 wa Kenya waliokwama Yemen wakirejea nyumbani kwa ndege ya Skyward Express iliyokodishwa.

Maofisa wa vyombo kadhaa vya usalama walimpeleka katika kituo cha polisi cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi.

“mmiliki wa hati ya kusafiria namba A2283881 na kitambulisho namba 0069184 ambaye alikuwa anatafutwa nchini Marekani kwa makosa yanayo husiana na ujangili wa pembe za ndovu na faru alikamatwa alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi”,vyombo vya usalama vilieleza.