Mahujaji hufutiwa dhambi zao, huwa kama wamezaliwa upya

AMEFARADHISHA Mwenyezimungu hijja kwa waja wake ili wapande daraja la ngazi ya twaa na utiifu ili hatimae wafikie katika takwaa ya mwenyezimungu  mtukufu. Uchamungu unaathari na mwenendo wa muislam, tabia zake na  muamala wake, kwani yeye anamwogopa mwenyezimungu na kujiepusha  na hasira zake na adhabu zake.

Hijja ni miongoni mwa ibada yenye kuleta matunda katika nafsi ya muumini aliye mcha mungu na matunda ya tabia nzuri na watu.

Anasema mwenyezimungu mtukufu (hija ni miezi maalumu basi ma mwenye kuhirimia hijja asifanye maasi wala vitendo vibaya na yoyote mnayofanya katika katika kheri fanyeni zawadi kwani ni ubora kumuogopa mwenyezi mungu.

Hivyo atakayeingia katika ibada ya hija na kuvaa ihiram pamoja na nia ni wajibu kwake aendane na tabia nzuri wala asifanye maasi wala kufanya mabaya wala mjadala katika hija.

Aidha, atapaswa kurekebisha nafsi na kuilea katika tabia nzuri pamoja na kuipamba mambo bora na kujiepusha na mabaya.

Anabainish Mtume (SAW) katika hadithi sahihi kwamba mwenye kushikamana na tabia nzuri kwenye hijja na akawa hakufanya maasi wala mambo mabaya na akawa na adabu, Hija yake itakuwa ni kifutio cha madhambi kwake kama aliyotanguliza, atarudi nyumbani kwake kama alivyozaliwa na mama yake, kutoka kwa Abi Hurairata (RA) anasema niemsikia Mtume (SAW) akisema (yeyote mwenye kuhiji na hakuasi na wala hakufanya mambo machafu atarudi kama siku alivyo zaliwa  na mama yake )

Na anasema Mwenyezi mungu mtukufu (na yote mnayoyafanya anayajua Mwenyezi mungu kwa maana chochote mtakachokifanya miongoni mwa twaa au sadaka au kuamrisha mema na kukataza mabaya, mwenyezi mungu anayajua na huu ni mwisho wa wakati wa hijja.

Na pale anapozowea mwenendo wa hija na kufanya vitendo vya kheri na kuacha mijadala na ugomvi na yale aliyoyatia sheriani Mwenyezi mungu katika hijja hayo yote ni kurekebisha na kuilea nafsi.

Kisha anasema Mwenyezimungu mtukufu (na fanyeni zawadi ni ucha mungu) na zawadi hapa ni kwa maana wema wa yale anayoweka akiba miongoni mwa mambo ya kheri na wema.

Yatakuwa ni yale yanayomkinga mtu na hasira za Mwenyezimungu na ghadhabu zake kwa vitendo vyo kheri na kujiepusha na mambo machafu na maasi.

Basi kwa mwendo hija afanye zawadi kwa yale anayo hitaji miongoni mwa matumizi chakula ili apatie sababu ya kisheria katika kuhifadhi maji ya uso wake ili kujiepusha na udhalili wa kuwa omba omba na ili asishughulike isipokuwa kumtaja Mwenyezimungu na twaa yake tu.

Vile vile matumizi yake yawe ya halali ili iwe hija yake imekubaliwa kwani mwenye viwanja vya hijja na ikawa matumizi yake ni ya halali na akasema (nimeitika ewe Mwenyezimungu nimeitika humwambia malaika umeitika na umefanikiwa.

Mungu akuzidishie vya haki na hija iwe yake imekuwabaliwa na utarudi kwa kulipwa na bila kupunguwa na hubakia mwenda hija afanye zawadi kwa ajili ya akhera kwa kumcha mungu na matendo mema kwani ubora awa zawadi ni kumcha na sikiliza maneno mya msemaji fanya zawadi katika uhai wako ni kwa ajili ya Mwenyezimungu.

Hivyo hajji anapaswa kukusanya zawadi nzuri na wala usiegemee dunia kwa wingi kwani mali inakusanywa na kwisha. Hivi unakubali marafiki wa watu wawe na zawadi na wewe ubaki bila ya zawadi.

Hivyo katika hija kuna utekelezaji wa amri ya Mwenyezi mungu mtukufu utekelezaji bora na kujibu utekelezaji wa wajibu ambao amefaradhisha Mwenyezi mungu mtukufu.

Amesema Mwenyezimungu mtukufu (Na watu wana wajibu kwenda kuhiji katika nyumba kongwe kwa wenye uwezo kwa njia zake na mwenye kukufuru kwa yakini Mwenyezimungu ni mkwasi kwa viumbe) na kisha akazidisha maana hii ya kutia nguvu herufu ya juu, kwani hapa kuna dalili ya wazi kwa wajibu juu ya waarabu kama atakaposema msemaji kwa Fulani kwangu kuna kadha na akataja Mwenyezimungu mtukufu hija kwa mambo ya ndani kabisa yanajulisha uwajibu.

Akasistiza haki yake na utukufu wa ukubwa wake na msemo wake huu umeenea kwa watu wote, hatoki humo isipokuwa yule iliyompita dalili kama mtoto, mtumwa,na katika hija mwenda hija anaishi muumini akiwa na nguvu kwa daraja la imani kwani humzuia kufikilia maasi bali hatakufikiria juu ya nyumba yake na nchi yake na Mwenyezi mungu mtukufu anasema

Na yule anayetaka kushikilia dhuluma tuta muonjesha adhabu imumizayo), (4) kwa maana ya mambo ya fedheha miongoni mwa maasi makubwa na makusudi na kwenye hija huhakikisha daraja la subira za aina tatu.

Subira juu ya twaa (Ibada), subira juu ya maasi na subira juu uwezo wa mwenyezi mungu kwa yale yanayo mpata mwenye kwenda hija miongoni mwa mashaka, taabu, kukosa mali na kuwa mbali na familia na marafiki zake.

Haya ni mazoezi ya matukio ya muislam juu ya subira na ibada na athari zake hudhihirika katika maisha ya muislam anaetekeleza faradhi hii. Aidha, hija ni shule kwa wenye k. kutojitolea na kutumia basi yeye anajifunza masomo katika kutoa na kujitolea hivyo basi imekuwa hija ni mlango miongoni mwa milango.

Sio mwenda hija huacha nchi yake na familia yake na marafiki zake pamoja na kujitolea mali zake kwa ajili ya kujisogeza kwa Mwenyezimungu. Hakika mwenda hija hufanya juhudi ya nafsi yake, anavua nguo zake na anajiepusha na kila na kila kitu kwa jili ya kumtii mwenyezimungu na kutekeleza amri zake.

Hii ni aina miongoni mwa aina ya jihadi ya mali na juhudi ya muda na katika hija. Kuna ukumbusho wa umauti na siku ya kukusanywa watu nayo inamkumbusha muislam siku ya kukutana na mwenyezimungu na haya nipale anapovua nguo mwenda hija na kuingia vazi la ihiramu na kusimama viwanja vya arafa, huku kukiwa na idadi ya watu wengi wakiwa katika vazi moja linazofanana na sanda.

Na hapa huja fikra katika kisimamo cha muislam baada ya vifo hivyo vyote humuita mtu katika kujiandaa na kifo na kuchukua zawadi kabla ya kukutana na mwenyezi mungu na katika hija humzoesha muislam kuviheshimu vyote vilivyo pembezoni mwake miongoni mwa miti na mawe nakadhalika.

Aidha husimama mipaka ya Mwenyezi mungu, haifai kwake kukata mti wala kuua kiwinda wakati wa kuhirimia hija, na wala kuokota kilichoanguka. Amesema Mwenyezi mungu mtukufu “Enyi ambao mlioamini musiue na nyinyi mkiwa katika hija na yeyote mwenye kuua miongoni mwenu kwa makusudi basi malipo yake ni kama kile alichokiua miongoni mwa wanyama.

Anahukumu hayo mwenye uadilifu kwenu kuchijwa au kafara (fidia) ya kulisha masikini ya kiasi chake kufunga ili aonje ubaya wa jambo lake.

Amesamehe Mwenyezi mungu kwa yote yaliyotangulia, na mwenye kurudia basi ataadhibiwa na mwenyezi mungu ni mshindi mwenye kuadhibu” (6).

Na kutoka kwa Ibni Omar (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema “Hakika Mwenyezi mungu ameharamisha vya haramu navyo ni haramu hadi siku ya kiama, haikatwi miti yake wala kung’olewa nyasi zake wala hakiokotwi kilicho dondoka isipokuwa kwa kutangazwa kwake na wala havihalalishwi viwindwa vyake” (7).

Basi mwenda hija anaepuka kwa kila lenye maudhi na muislam katika hija anajisikia undugu wa kiislam na usawa katika kisimamo chake cha arafa na vinginevyo miongoni mwa visimamo na ndugu zake waislam pamoja na kutofautiana kwa lugha zao, utaifa wao na rangi zao.

Wapo katika kiwanja kimoja na vazi moja hapana tofauti kati ya rais na raia na kati ya mkubwa na mdogo na kati ya tajiri na masikini.

Wote wanasema labaika, na takbira na wananyenyekea kwa mwenyezi mungu kwa nyoyo zenye unyenyekevu na wakinyoosha mikono kwa kuomba dua na ndimi zimejaa tajo la Mwenyezi mungu na sifa zake, katika yale yanayokuwa ni sababu ya kuvutia rehema zake na kufuta makosa.

Hapo hujisikia mwenda hija maana ya usawa wa uhakika nako ni kwamba wote wanauhakika nako ni kwamba wote wanatarajia rehema za Mwenyezi mungu na wananyenyekea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Basi tajiri na masikini, mwenye mali na mnyonge, mdogo na mkubwa wote ni watumwa wa mwenyezi mungu wenye kuhitajia kwake.

Hapo hujihisi udugu na usawa na kuhakikisha kwamba uma wa kiislam ni uma mmoja, hapa huanguka alama mbaya za kuufara kuanisha umma na kuhakikisha uma ulioparaganyika uaningia katika msimu wa hija.

Mwenyezimungu mtukufu anasema “Hakika huu uma wenu ni uma mmoja na mimi ni mola wenu basi niogopeni” (9). Hata kama umma umefarikiana, hija hubatilisha haya yote.

Hizi ni baadhi za athari za hija katika nafsi ya muumini isipokuwa athari hizi hazifungamani kwa mtu isipokuwa atakapo rudi mwenda hija akiwa amebadilika mwenendo wake na muamala wake.

Kauli ya Mtume  (SAW) amesema, “Hija iliyokubalika haina malipo isipokuwa pepo” na kauli yake (SAW) “atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi mungu wala hakufanya maasi wala mabaya atarudi kama alivyozaliwa na mama yake” (17) kwani yeye atakuwa ni mwepesi na mwenye kujua mno juu ya kupata daraja hili kubwa na haja anaporudi kwenye jamii yake na nchini kwake, atarudi na tabia za wachumungu na matendo ya watu wema.

Aidha atarudi hali ya kuwa  na ibada za waumini wacha mungu kwani yeye ameishi katika uchamungu alipokuwa hija, kwa mwenendo na ibada na tabia.  Imepokelewa kuwa miongoni mwa alama ya hija iliyokubaliwa ni kulisha chakula na ulaini wa maneno na tabia njema na hivi ndivyo anavyotakiwa mwenda hija kuirekebisha nafsi na kunyoosha mwenendo na kumpelekea kupambika navyo hivyo vyote.

Hivyo, tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie matendo yetu mema na atuwafikishe kila la kheri ewe mwenyezi mungu mpe rehema na amani mtume wetu Muhammad (SAW) na jamaa zake na sahaba zake salam nyingi, na shukurani zote anastahiki Mwenyezi mungu mola mlezi wa ulimwengu.