KIGALI,RWANDA

USAFIRI  wa ndege nchini Rwanda unatarajiwa kuanza tena mwezi Ogasti mwaka huu baada ya kuzuiliwa kwa muda kutokana na janga la Covid-19.

Nchi mbali mbali duniani zinafungua tena na kuruhusu mashirika ya ndege ya kibiashara, ambayo yalikuwa yamesimamishwa miezi mitatu iliyopita.

Rwanda ilitangaza kufunguliwa kwa uwanja wake wa ndege wiki iliyopita, ikiruhusu mashirika yote ya ndege kuanza shughuli zake chini ya hatua za za usalama wa afya zilizowekwa na Wizara ya Afya.

Meneja wa oparesheni hiyo,ofisi ya Satguru Travels Rwanda, Swapnil Karkhile aliliambia gazeti la New Times kuwa wanafuatilia taarifa kutoka mashirika ya ndege ili kukamilisha mipango ya safari.

Shirika la ndege la Ethiopia lilianza tena safari za ndege wiki iliyopita, na kuongeza ndege nyengine Zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasafiri.

Ndege ya Brussels Airlines,ilitangaza kuwa itaanza safari za ndege katika maeneo tofauti ikijumuisha Kigali.

Hata hivyo,Everard alisema kuwa mpango wa kusafiri kwa kipindi hichi cha kufunguliwa unategemea mabadiliko kulingana na mahitaji yaliyopo.

Ndege kubwa zaidi ya ulimwengu, Qatar Airways, ilipanga kuanza safari za ndege kwenda Kigali mnamo Agosti 3, na ilikusudia kuruka mara tatu kwa wiki .

Ndege hiyo hapo awali ilikuwa ikifanya kazi kila siku kwenda Kigali, lakini kwa athari ya janga hilo, Viwanja vya ndege vya Qatar vinapungua kwa ndege kwani mahitaji ya kusafiri kwa ndege yalipungua.

“Hatutarajii biashara hiyo kurudi katika hali yake ya kawaida kwa haraka kwani bado tuna wasi wasi wa Covid-19”,alisema.

Hata hivyo  alisema wakati mashirika ya ndege yakianza tena shughuli zake ,kipaumbele Zaidi kitapewa wateja ambao tayari waliweka bookings.