NAIROBI,KENYA

OFISI za Chama cha Kitaifa cha Amani (ANC) katika Kaunti ya Kakamega zimeteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana.

Ofisi ya Kakamega ni mahali ambapo hati nyingi za chama huhifadhiwa ikiwa ni pamoja na usajili wa wanachama wake.

Kwa mujibu wa shahidi aliyekuwepo karibu na eneo la tukio Patrick likanamon alisema,tukio hilo lilitokea jana asubuhi.

Washirika wa chama ambao walikuwa wameanza kuondoka eneo hilo sasa wanashutumu wapinzani kwa kusababisha moto kama njia ya vitisho.

Hadi sasa kuna mabango yalichomwa na hati nyengine chache,lakini hati za usajili wa chama hazijachomwa.