WAPENZI wasomaji wetu wa gazeti hili pendwa, kwanza niseme Balakat el eid, nawatakia sikukuu njema waislamu wote waliomaliza kufunga mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Ijumaa ijayo ni sikukuu ya eid el Hajj (Eid El adhaa) ambapo waislamu wote duniani wanasherehekea kumaliza kwa ibada ya hijja inayotarajiwa kukamilika wiki hiyo huko Makka nchini Saudi Arabia.
Hivyo basi waislamu kwa kawaida hutayarisha milo muhimu na adimu kwa ajili ya siku hiyo.
Basi katika safu yetu hii ya maakuli nimewatayarishia pishi pambe la mchana yaani Biriani ya kuku.
Upishi huu ili kukamilika ni lazima uwe na vifaa na vipimo, namna ya kupika na mahitaji ya chakula hichi kwa ujumla wake.
VIPIMO NAMNA YA KUMPIKA KUKU
Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu
Kuku (Mkate kate Vipande) – 4 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 Vijiko vya supu
Chumvi – kiasi
Pilipili nyekundu ya unga – 1 Kijiko cha supu
Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) – 1 Kijiko cha chai
Bizari ya pilau ya powder (Jeera) – 1 Kijiko cha chai
Gilgilani powder (Dania) – 1 Kijiko cha chai
Ndimu – 1 Kijiko cha supu
MCHELE NA VITU VYA MASALA:
Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) – vikombe 7
Mafuta ya kupikia – kiasi
Vitunguu Vilivyokatwa – 8
Tungule iliyokatwa katwa – 3
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 1 Kijiko cha supu
Pilau Masala -1 Kijiko cha supu
Hiliki powder – ½ Kijiko cha chai
Tomatoe paste – 1 Kijiko cha supu
Pilipili mbichi zipasue katikati – 4
Chumvi – kiasi
Mtindi – 4 Vijiko vya supu
Kotmiri iliokatwa (Chopped) – ½ Kikombe
Mafuta ya kunyunyuzia katika wali – 3 Vijiko vya supu
Zaafarani au rangi ya biriani – kiasi
NAMNA YA KUTAARISHA NA KUPIKA
Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome mpaka awive na awe mkavu kiasi.
Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.
Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.
Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.
Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.
NAMNA YA KUPIKA WALI WA BIRIYAN
Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.
Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.
Weka katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa dakika 15 – 20. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.
VIDOKEZO UKIPENDA
Mtindi wa kutolea Biriyani:
Mtindi – 1 kikombe
Pilipili mbichi – 1 ndogo
Kitunguu saumu(/galic) thomu – chembe mbili
Nanaa – kiasi
Chumvi – chembe tu
Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli