LONDON, England

MENEJA wa klabu bingwa England, Liverpool FC, Jurgen Klopp amesema wachezaji wake wanatakiwa kujifunza kwa kilichotokea katika mchezo dhidi ya Arsenal ambapo wamepoteza nafasi ya kuvunja rekodi ya Manchester City.

Kikosi cha Klopp ambacho kinatarajiwa kukabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya mchezo dhidi ya Chelsea juma lijalo, ilikua na nafasi ya kuvunja rekodi ya misimu miwili iliyopita iliyowekwa na Manchester City kwa kumaliza msimu huo wakiwa na pointi 100 kibindoni.