TURIN, Italia
CRISTIANO Ronaldo amefunga penalti mbili huku Juventus ikilazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Atalanta kwenye mechi ya ‘Serie A’ na kuendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi nane.
Wageni, Atalanta ambao walimiliki mchezo kwa kipindi kirefu, waliongoza mara mbili mjini Turin kupitia kwa Duvan Zapata na Ruslan Malinovskiy.
Hata hivyo, Ronaldo ilimchukua kufikisha jumla ya magoli 28 kwenye michezo 28 ya ligi kwa kufunga mkwaju wa penalti katika dakika ya 90.
Lazio inayoshika nafasi ya pili ilikumbana na kipigo cha magoli 2-1 nyumbani mbele ya Sassuolo.
Atalanta, ambayo imeshafunga mabao 19 zaidi ya timu nyengine yoyote katika ligi hiyo ya juu ya Italia msimu huu, ilionekana kama imengelipanda hadi ya pili kwenye msimamo na ushindi wa 10 mfululizo kabla hali kugeuka.(AFP).
RONALDO aiokoa na kipigo Juve
