KIGALI, RWANDA

OFISI ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) juzi imesema kuwa imelikamata gari lililokuwa na watu 57 wanaodhaniwa ni kundi la waasi kutoka msitu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Watuhumiwa hao, waliyokamatwa na wanajeshi wa DRC, walituhumiwa kwa ugaidi na kuunda vikundi vya wenyeji ili kukabiliana na Rwanda.

Kaimu msemaji wa RIB Dominique Bahorera alisema hayo muda mfupi baada ya watuhumiwa hao kufikishwa mbele ya waandishi wa habari katika mji mkuu wa Rwanda Kigali.

“Walikuwa wa vikundi tofauti vya kigaidi vilivyoko DRC, kama vile National Liberation Front (FLN), Kikosi cha Kidemokrasia cha Ukombozi wa Rwanda, na Harakati ya Rwanda ya Mabadiliko ya Kidemokrasia”, alisema Bahorera.

Hata hivyo, taarifa zilisema kuwa washukiwa hao walikabidhiwa nchini Rwanda katika mfumo wa ushirikiano wa usalama kati ya nchi hizo mbili, kwa mujibu wa RIB.

Mwaka jana, DRC na nchi za kikanda zilikutana kushughulikia vikundi vyenye silaha vilivyofanya kazi nchini DRC, ambazo zimekuwa zikitishia usalama wa mkoa huo kwa muongo mzima.