KIGALI,RWANDA

RWANDA imekusudia kuweka masharti magumu kwa taasisi zote za masomo ya juu na wawekezaji kwenye sekta hiyo ili kuhakikisha kuwa elimu bora inapatikana.

Dk Rose Mukankomeje

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Elimu ya juu (HEC), Dk Rose Mukankomeje, alielezea kwamba hatua hiyo inatokana na ukaguzi wa hivi karibuni unaofanywa na taasisi yake.

Hatua hiyo inakuja baada ya Wizara ya elimu kufunga vyuo vikuu vitatu vya kibinafsi kutokana na kile ilichosema ni changamoto za kiutawala ambazo zinaathiri ubora wa elimu.

Kulingana na HEC, maamuzi yaliyopendekezwa yatakuwa magumu lakini yatakuwa na lengo la kuboresha ubora wa elimu.

Mukankomeje alisema kuwa kati ya kanuni zinazotekelezwa ni kuwalazimisha wawekezaji binafsi kutumia fedha za usawa isipokuwa mikopo ya benki kufungua vyuo vikuu vya kibinafsi.

Maamuzi mengine madhubuti ni pamoja na kumtaka mwekezaji kuweka mpango endelevu wa uwezo wa kifedha ili kuwalipa wafanyakazi kwa muda huo bila kutegemea mkopo na masomo ya wanafunzi kabla ya kuruhusiwa kuanzisha chuo kikuu cha kibinafsi.

Taasisi zote za masomo ya juu nchini zilipewa muda hadi hadi Ogosti 15 kuwasilisha uthibitisho wa maendeleo yao ya kifedha kwa halmashauri ya elimu ya juu (HEC) au kufungwa kwa hatari.

“Tunajipanga pia kuajiri wafanyakazi zaidi ili kuimarisha mchakato wa ukaguzi wa vyuo vikuu.Hizi sheria mpya za ukaguzi zitakuwa na uvumilivu kwa wasiotimiza mashsrti”,alisema Mkurugenzi.

“Kumekuwa na kutokuelewana sana katika vyuo vikuu vilivyofungwa, wamiliki wanaingilia kati katika idara za utawala na uhasibu, wanachukua pesa zilizolipwa na wanafunzi na wanakataa kununua mahitaji ya kimsingi yanahitajika skuli,” Dk Theoneste Ndikubwimana, Mkuu wa ubora wa masomo alisema.

Chuo Kikuu cha Kikristo cha Rwanda na Chuo cha elimu cha Indangaburezi mwezi huu kilifungwa kwa madai ya changamoto za kiutawala ambazo zinaathiri ubora wa elimu.