KIGALI, RWANDA

WIZARA  ya Afya Rwanda imetangaza kuongeza idadi ya vitendea kazi  nchini kabla ya mwisho wa Julai mwaka huu ili kupambana na Covid-19.

Waziri wa Afya Dk. Daniel Ngamije,akizungumza katika kikao cha Bunge kuhusu wasi wasi wao kwamba Serikali ina miundombinu muhimu ya kuwatibu wagonjwa wa Covid-19 ambao wako katika hali mbaya alisema jambo hilo limezingatiwa.

Alisema hadi sasa nchi ina vianzio 60 ambavyo vilipelekwa katika vituo tofauti kwa ajili ya kutumika kutibu wagonjwa wenye hali mbaya ikiwa hadi sasa Wizara hiyo inatarajia kuwa na vianzio 200 zaidi mpaka kufikia mwisho wa mwezi huu. 

Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza utayari wa nchi hiyo katika kuwatibu wagonjwa wa Covid-19 waliopo katika hali mbaya na shida ya kupumua.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Biomedical Rwanda (RBC) Dk Sabin Nsanzimana,aliliambia gazeti la New Times kwamba wagonjwa wanne tu ndio waliotibiwa kwa kutumia viingilizi tangu kuzuka kwa janga hili katikati ya Machi.

Kwa sasa hali ni tofauti na Machi wakati nchi ilipokuwa na maabara moja ya kushughulikia vipimo vya Covid-19, ikiwa kwa sasa Rwanda ina maabara zaidi ya saba za kupimia Covid-19 pamoja na vituo 17 vya matibabu vyenye uwezo wa kutibu watu 1,767.

Wizara ya Afya hivi karibuni ilitangaza kutumia kiasi cha dola milioni 60 (zaidi ya bilioni Rwf44) katika mapambano dhidi ya Covid-19 tangu Machi.

Serikali pia inafanya miradi ya kutumia zaidi ya dola milioni 13 hadi Septemba mwaka huu.