NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya Simba kinatarajia kushuka kwenye Dimba la Mkwakwani Tanga leo kuvaana na Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Wekundu hao wa msimbazi jana wamefanya mazoezi yao ya mwisho kwa ajili ya kuwakabili Coastal Union.

Simba SC leo wataingia Mkwakwani na kombe lao mkononi kwa ajili ya kuwaonyesha  mashabiki wao wa Tanga.

Hivi karibuni kocha mkuu wa timu hiyo Sven Vandenbroeck, alisema lengo lao nikumaliza vizuri michezo yao iliyobakia.

Alisema wanakwenda kupambana kupata pointi kama ambavyo wamekuwa wakipambana kwenye michezo yao mingine.

“Tunaendeleza tulipo ishia lengo letu nikufanya vizuri kwenye kila mchezo,” alisema

Kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao hao huku mabao yote yakifungwa na Gerson Fraga kipindi cha kwanza.