Watumishi waliodaiwa kuiba wafikishwa ZAECA

NA ASIA MWALIM

WAKALA wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), imeyafungia maduka mawili ya dawa, vipozi ya watu binafsi baada ya kugundulika kuuza dawa za Serikali.

Mfamasia Msimamizi wa Wakala na Usalama wa Dawa, Chakula na Vipodozi (ZFDA), Nassir Buheti, aliyasema hayo wakati akizungumza na Zanzibar leo, huko ofisini kwake Mombasa mjini Unguja.

Alisema dawa hizo za Serekali zilikamatwa kwenye maduka ya wafanyabiashara binafsi, wakiwa katika harakati ya kuziuza dawa hizo kama bidhaa nyengine, ambapo jambo hilo ni kinyume na sheria.

Alisema ZFDA, imefanya ukaguzi kwenye maeneo tofauti ya maduka ya kuuzia dawa na kufanikiwa kukamata kiasi cha dawa chenye wingi wa aina 14 na zilikamatwa maeneo Nyamanzi na na Mwanyanya Mjini Unguja.