Hazina uhusiano wa corona

NA ABDI SULEIMAN

UWEPO wa ugonjwa wa Covid 19 nchini Tanzania sio sababu ya kutokupelekwa watoto katika vituo vya afya kutokupatiwa huduma za chanjo kikamilifu.

Hayo yameelezwa na Mratib wa kitengo cha chanjo Zanzibar Dr. Abdullhamid Ameir Saleh, wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari Pemba, wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi kuhusu Chanjo.

Alisema katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Covid 19, mwamko wa wananchi umekuwa ni mdogo katika kuwapeleka watoto wao kupata huduma za Chanjo, ikizingatiwa Chanjo zinamkinga mtoto na magonjwa mbali mbali.

Mratib huyo alifahamisha kuwa, Tanzania haina mpango wowote wa kufanya majaribio ya chanjo ya Covid 19 kwa wananchi wake, kwani chanjo zilizopo vituoni hazina madhara yoyote kwa binaadamu.

“Ndugu zangini wasiwasi na hofu ondowenu juu ya kitu hicho, chanjo ya ugonjwa huo haipo mapka sasa, wala wadudu wa virusi hawana chanjo tafauti na wadudu wengine wakiwemo bektiria hawa napatikana chanjo zao,”alisema.

Aliwataka wananchi kufahamuwa chanjo ya Corona bado haipo na hakuna yoyo iliyofanyiwa majaribio na kuthibitishwa na shirika la Afya Duniani(WHO) kuwa inatibu ugonjwa wa Corona.

“Chanjo za virusi ni vigumu kuchanganywa na kuwa moja, lakini chanjo za baktiria zinaweza kuchanganywa na kutumika, waanchi katika vituo cya Chanjo,”alisema.