FREDY MGUNDA, MUFINDI
USHIRIKIANO baina na Serikali ya Wilaya ya Mufindi na Shirika la kuhudumia watoto SOS umesaidia kuimarsha uchumi wa kundi la wanawake vijijini wakiwemo wajane waliokuwa wakikabiliwa na hali duni ya kipato na kushindwa kuhudumia familia.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Robert Sungura, alisema mradi wa uwezeshaji wanawake kiuchumi umesaidia wanawake walio wengi kujiongezea kipato kwa kuanzisha shughuli za ujasiriamali ikiwemo kilimo biashara
Miongoni mwa wanawake wa kikundi cha akina mama Wajane cha kijiji cha Iyela wakizungumza wakati wa ukaguzi wa shughuli za maendeleo ya vikundi wameeleza kuwa uwezeshwaji huo umewasaidia kukidhi mahitaji ya familia.
Jumla ya Kaya 250 za wanawake wajane zinazolea watoto wapatao 928 Wilayani Mufindi Mkoani Iringa, walisema muda mwingi walikuwa wakitaabika juu ya malezi ya watoto walioachiwa na wenzi wao waliotangulia mbele za haki.
Wanawake hao walisema kuwa wamefaidika na mradi uwezaji wanawake kiuchumi unao fadhiliwa na Shirika la Kuhudumia watoto SOS Childrens Village Tanzania kwa Kilimo cha Nyanya na Mahindi, ambacho kimebadilisha maisha ya Akinamama hawa wa Kijiji cha Iyela ambapo kimewafanya waweze kusomesha watoto, kujenga Nyumba na Kuongezeka kwa Mazao kupitia elimu bora ya kilimo cha kisasa.