KHARTOUM,SUDAN
SUDAN imetangaza hali ya dharura katika eneo linalokumbwa na machafuko la magharibi mwa Darfur baada ya vurugu kutokea katika miji miwili.
Hayo yaliripotiwa na shirika la habari linalomilikiwa na serikali SUNA.
Ujumbe wa pamoja wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa (UNAMID), ulisema umetuma timu katika mji wa Kutum, kaskazini mwa Darfur, kufuatia ripoti kwamba kituo cha polisi pamoja na magari yalichomwa moto na watu wasiojulikana.
Hata hivyo ujumbe huo haukutoa taarifa zaidi,Maandamano ya amani yalikuwa yakifanywa Darfur na maeneo mengine ya Sudan dhidi ya uwepo wa makundi yenye silaha.
Baraza la mpito linalojumuisha raia na wanajeshi ambalo limekuwa likiongoza serikali tangu Rais Omar al-Bashir alipong’olewa madarakani, limeapa kumaliza machafuko hayo, na pia kufanya mazungumzo na baadhi ya makundi ya waasi ambayo yalipambana dhidi ya serikali ya Bashir eneo la Darfur na kwingineko.