NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam, imeokoa kiasi cha fedha zaidi ya Shilingi Milioni 56  robo mwaka kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu.

Fedha zilizookolewa ni kutoka katika  Vyama vya Saccos ,matumizi ya mashine za kukusanya mapato za Manispaa.

Alisema watu wamekua wakikusanya mapato hayo kwa kutumia kwa kutopeleka Benki na badala yake wanakusanya na kufanya matumizi yao binafsi.

Hayo yalisemwa Jana  Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, na  Eugenius Hazinamwisho, alisema kuna Idara zinaongoza kulalamikiwa ni pamoja na Tamisemi, Idara Binafsi, Polisi na Mahakama.

Alisema kuwa vitendo vya rushwa  ya  ngono vyuoni pamoja  na shule alisema rushwa ya hiyo ina changamoto sana kutokana na  kugubikwa na aibu msichana akiombwa rushwa ya ngono anashindwa kutoa taarifa, huku akitoa wito kwa wasichana waamke wasikubali kukaa kimya ili kutokomeza vitendo hivyo.