NA SAIDA ISSA, DODOMA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) imeunda tume huru toka nje ya taasisi hiyo itakayochunguza matumizi ya pesa yaliyotumika Katika Majengo Saba Pamoja na kuchunguza iwapo Kuna ubadhirifu ,wizi au rushwa zilizotumika Katika ujenzi huo.

Majengo hayo ya TAKUKURU yapo Katika wilaya za Chamwino na Mpwapwa Mkoani Dodoma, Ngorongoro Mkoani Arusha, Manyoni Mkoani Singida,Masasi Mkoani Mtwara, Namtumbo Mkoani Ruvuma Pamoja na Ruangwa Mkoani Lindi.

Hatua hii imekuja kufuatia hoja za mapendekezo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli dhidi ya taasisi hiyo yaliyolenga kuondoa madoa ya uwepo wa viashiria vya rushwa.

Hivi karibuni Rais Magufuli wakati wakati akizindua jengo la TAKUKURU ngazi ya wilaya lililopo Katika wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma aliiagiza taasisi hiyo kuona haja ya kujitathimini kwa dhidi ya tuhuma za  viashiria vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wake .

Akiongea na vyombo vya habari Jana Jijini hapa, MKURUGENZI mtendaji wa TAKUKURU Brigedia Jenerali  John Mbungo, alisema taasisi hiyo imeunda timu itakayotokana  na wajumbe wanne kutoka maeneo ya Contractors Registration Board, Suma Constraints company limited na Tanzania Building Agency.

“Uchunguzi huu utafanyika kwa siku kumi na nne kuanzia Sasa na tuhuma zozote zitakazothibitika zitachukuliwa hatua Kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo,”alisema.