NA HANIFA SALIM
NAIBU Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wanawake, Wazee na Watoto, Shadya Mohamed Suleiman ameongoza kwa kupata kura 96 katika mchakato wa uchaguzi wa viti maalum nafasi ya uwakilishi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Kusini Pemba.
Shadya alifuatiwa na Zuhura Mgeni Othman aliepata kura 58 na Zainab Omar Amir aliepata kura 55.
Kwa upande ubunge Maryam Azan Mwinyi aliongoza kwa kura 64, akifuatiwa na Zulfa Mmaka Omar aliepata kura 62 na Nadra Gulam Rashid alipata kura 52.
Nafasi za viti maalumu wasomi (ubunge)
walioshinda ni Fatma Juma Suleiman aliepata kura 104, Hadia Miraj Ame alipata
kura 30 wakati kwa upande wa uwakilishi Maryam Said Khamis alipata kura 83 na
Aisha Abdi Juma alipata kura 49.
Kwa upande wa nafasi za watu wenye mahitaji
maalumu (ubunge), Hidaya Mjaka Ali alipata kura 128, nafasi ya uwakilishi Raya
Suleiman Hamad alipata kura 60, Aisha Ali Abdalla
kura 36, Hidaya Idris Juma kura 31 wakati
nafasi ya NGOs Saumu Saleh Abdalla
alipata 128.
Kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, viti maalumu uwakilishi, Bihindi Hamad Khamis alipata kura 59, Chumu Kombo Khamis alipata kura 56 na Faida Hamad Juma alipata kura 44.
Nafasi ya ubunge viti maalumu mkoa huo, Maida
Hamad
Abdalla alipata kura 99, Asia Sharif Omar
alipata kura 66 na Raiya Amour Othman alipata kura 52,wakati viti maalum watu
wenye ulemavu uwakilishi Fatma Ramadhan Shaibu alipata kura 49, Hijra Halfan
Hamad alipata kura 43 na Awena Khamis Rashid alipata kura 23.
Katika nafasi ya ubunge viti maalumu watu wenye
ulemavu, Asha Omar Saidi alipata kura 124 ambae hakuwa na mpinzani.
Mapema akizungumza, Mjumbe wa kamati ya siasa Hemed Suleiman Abdalla, aliwataka
wajumbe kutowachagua watu ambao wamefanya
siasa chafu na kutoa rushwa kwa ajili ya
kupigiwa kura.
Alisema wagombea wote ambao wamejitokeza kuwania nafasi hizo wanatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi hivyo lazima wawe watulivu, nidhamu huku wakifuata utaratibu wa uchaguzi.
“Msichague mtu alietoa rushwa na wapo ambao wanafanya siasa chafu katika jamii, nasema chama kwanza mtu baadae tuchague viongozi ambao wataleta maslahi ya chama,” alisema.