Kepa Arrizabalaga
SEVILLA wanajiandaa kufanya uhamisho wa mkopo wa mlinda mlango wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga (25), ambaye mustakabali wake haujajulikana Stamford Bridge. (Sun).

Lucas Digne
KLABU za Chelsea na Manchester City zinaweza kugeuka kwenye mpango wa kumnasa beki wa kushoto wa Everton, Mfaransa Lucas Digne(26), ikiwa itakuwa vigumu kumpata Ben Chilwell (23), anayekipiga Leicester. (ESPN).

Leon Bailey
KLABU za Everton, Liverpool, Manchester City na Manchester United zinatarajia kumshuhudia, Leon Bailey (22), wakati ambapo winga huyo wa Bayer Liverkusen akiwa na matarajio ya kuhamia England. (Sky Sports).

Kalidou Koulibaly
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amewaorodhesha wachezaji wa nafasi ya ulinzi ya Napoli, Msenegali Kalidou Koulibaly (29), Pau Torres wa Villarreal (23), na nyota wa Benfica, Mholanzi Ruben Dias (23), akitarajia kufanya mabadiliko safu yake ya ulinzi. (Times).

Eric Bailly
MANCEHESTER United wapo tayari kumruhusu, Eric Bailly (26), kuondoka kwa mkopo msimu ujao wakati Valencia ikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi. (Sun).

Dean Henderson
MLINDA mlango anayechezea Manchester United kwa mkopo, Dean Henderson (21), ameitahadharisha klabu kuwa hatasubiri milele kuwa chaguo lao la kwanza, kauli hiyo imekuja wakati Chelsea ikionesha nia na mchezaji huyo. (Express).

Mike Maignan
CHELSEA inamfuatilia mlinda mlango wa Lille, Mike Maignan (24) na Alphonse Areola (27) anayecheza kwa mkopo Real Madrid akitokea Paris St- Germain. (Express).

Hugo Lloris
KLABU ya Tottenham pia wanafikiria kumnyakua, Magnan huku kocha Jose Mourinho akimtolea macho mchezaji huyo kuwa mrithi wa mlinda mlango wa sasa, Hugo Lloris. (33). (Sun).

Jack Grealish
KOCHA wa zamani wa Aston Villa, Tim Sherwood anaamini nahodha, Jack Grealish (24), atajiunga na Manchester United msimu huu. (Birmingham Mail).

Giovani Lo Celso
KOCHA Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho, amesema hatambadilisha, Giovani Lo Celso (24) kwa Bruno Fernandes wa Manchester United, baada ya Spurs kumkosa kiungo huyo msimu uliopita. (Sky Sports).

Abdul Mumin
KLABU ya Sheffield United ingelipenda kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Abdul Mumin (22) kutoka FC Nordsjaelland msimu huu. (Mail).

Filip Kostic
KIUNGO, Filip Kostic (27), anaweza kuondoka Eintracht Frankfurt, huku InterMilan na klabu za Ligi Kuu ya England zikiwa zinamtolea macho winga huyo raia wa Serbia. (Goal ).