Pierre-Emerick Aubameyang
ARSENAL wanajiandaa kumpatia mkataba mpya mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang (31), unaokadiriwa kuwa pauni 250,000 kwa wiki pamoja na marupurupu mengine katika juhudi za kumshawishi asiondoke klabu hiyo. (Telegraph).

Donny van de Beek
KOCHA wa Ajax, Erik ten Hag, amesema kiungo ambaye pia ananyemelewa na Mancehster United, Donny van de Beek (23), anaweza kuondoka mara dirisha la usajili litakapofunguliwa tena.(Mirror).

Steve Gerrard
MENEJA wa Rangers, Steven Gerrard (40), amekata ofa ya kuwa meneja mpya wa Bristol City. (Bristol Post).

Milot Rashica
KLABU ya Borussia Dortmund wameanza mchakato wa kumsaka winga wa Werder Bremen na Cosovo, Milot Rashica (24), huku wakimtafuta atakayejaza pengo litakaloachwa na mshambuliaji wa England, Jadon Sancho (20), ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Telegraph).

Kepa Arrizabalaga
VALENCIA wanajiandaa kumnunua kipa wa Chelsea na Hispania, Kepa Arrizabalaga (25), pamoja na mchezaji nyota wa Manchester City Muhispania, David Silva (34). (90min).

Leroy Sane
WINGA wa Bayern Munich, Leroy Sane (24), amemsihi beki wa Austria, David Alaba (28), kusalia katika klabu hiyo badala kurejea tena Manchester City au kwenda Real Madrid. (Sport Bild).

Japhet Tanganga
MLINZI wa England, Japhet Tanganga (21), anakaribia kusaini mkataba mpya naTottenham. (Evening Standard).

Pierre-Emile Hojbjerg
KLABU ya Tottenham wanaamini watafanikiwa kumsaini kiungo wa Southampton na Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg (24), licha ya dau la Everton la pauni milioni 25 kukubaliwa. (Guardian).

Kai Havertz
BAYERN Leverkusen huenda wakaamua kumsaini kwa mkataba wa mkopo kiungo wa Real Madrid na Brazil chini ya umri wa miaka 23, Reinier (18), ikiwa mshambuliaji wa Ujerumani, Kai Havertz (21), atahamia Chelsea. (Goal).

Douglas Luiz
KLABU ya Arsenal wanataka kumnunua kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz (22), lakini, Manchester City huenda wakamnunua tena mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (90min).