Edinson Cavani
BENFICA imesitisha azma yake ya kumsaka mshambuliaji, Edinson Cavani (33), huku mshambuliaji huyo aliyekuwa Paris St-Germain akidai karibu pauni milioni 18 kwa kila msimu. (A Bola).
Jose Gimenez
CHELSEA imekuwa ikimfuatilia mlinzi wa Atletico Madrid na Uruguay, Jose Gimenez (25), huku kocha Frank Lampard akiwa anafuatilia kutatua mapungufu ya upande wa ulinzi wa kikosi chake. (Telegraph).
Leroy Sane
WINGA, Leroy Sane (24), alionekana kuthibitisha wakati anatambulishwa Bayern Munich kwamba mchezaji mwenzake wa Ujerumani, Kai Havertz (21), anakwenda Chelsea kutoka Bayer Leverkusen msimu huu.(Goal).
Kai Havertz
CHELSEA na ajenti wa Kai Havertz wamefikia makubaliano ya kibinafsi kwa ajili ya kiungo huyo wa Leverkusen. (Nicolo Schira).
Ben White
KLABU ya Brighton haina mpango wowote wa kumuuza mlinzi wa Uingereza, Ben White (22), kwa Leeds United ambapo amekuwa kwa mkopo msimu huu. (Mail).
Jesse Lingard
KIUNGO, Jesse Lingard (27), amemtaka kiungo mwenzake wa Uingereza, Jadon Sancho (20), kuondoka Borussia Dortmund na kujiunga naye Manchester United msimu huu. (Evening Standard).
Thiago Alcantara
KLABU ya Bayern Munich imesema kiungo raia wa Hispania Thiago Alcantara (29), hataruhusiwa kuondoka kiurahisi baada ya kuhusishwa kuhamia Liverpool. (Metro).
Ferran Torres
KLABU ya Valencia imesimama kidete kwa malipo inayotaka kwa winga, Ferran Torres (21), huku Manchester City ikiwa makini kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania chini ya umri wa miaka 21. (Telegraph).
Ed Woodward
NAIBU mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward anafikiria kumteua mkurugenzi wa soka katika klabu hiyo msimu huu. (Telegraph).
Nicolo Zaniolo
KLABU ya Tottenham inamfuatilia kiungo wa kati wa Roma na Italia, Nicolo Zaniolo (21), ambaye wanapania kumsajili.(Goal).
Eberechi Eze
WEST Ham imemuweka kiungo wa Queens Park Rangers, Eberechi Eze (22), kama mchezaji wa kwanza wanayemlenga wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa huku Crystal Palace pia nayo ikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 20. (Evening Standard).
Dennis Bergkamp
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Uholanzi na Arsenal, Dennis Bergkamp amesema atakuwa tayari kurejea klabu hiyo kama kocha siku za usoni. (FourFourTwo).