Denis Zakaria
CHELSEA wanaangalia kusaini nyota wa kimataifa wa Uswisi, Denis Zakaria, lakini, kwanza wataangalia kumpata Kai Havertz.
Zakaria (23), amekuwa sababu kubwa ya kuongezeka kwa Gladbach katika nne za juu na pia anatafutwa na Manchester United na Manchester City.(Goal).

Sergio Romero
MLINDA mlango wa Manchester United, Sergio Romero, ameibuka kama mlengwa wa uhamisho kwa Everton na Leeds.
Klabu zote mbili zinaweza kuzindua zabuni za majira ya joto kwa nyanda huyo wa Argentina, ambaye amechanganyikiwa na jukumu lake kwenye ikosi cha Ole Gunnar Solskjaer nyuma ya David de Gea.(ESPN).

Sandro Wagner
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Bayern Munich, Sandro Wagner ametangaza uamuzi wake wa kuondoka Tianjin Teda.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye alihamia Ligi Kuu ya China mnamo Januari 2019, ametumia muda wake mashariki ya mbali kwa sababu za kifamilia.(Be Soccer reports.).

Rafinha
KLABU ya Barcelona ipo tayari kumuuza kiungo wa Brazil, Rafinha kwa Inter Milan.
‘Blaugrana’ walikataa ofa ya euro milioni 10 kutoka kwa Celta Vigo kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 mapema mwezi huu, lakini, sasa wapo tayari kukubali ombi la Nerazzurri la euro milioni 16.(Mundo Deportivo).

Jeremie Boga
KIUNGO wa Sassuolo, Jeremie Boga ndiye mlengwa wa azma kutoka Napoli na Marseille.
Marseille wanahitaji kupata fedha kabla ya kuzindua ofa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini, Napoli tayari ameandaa ofa ya dola milioni 25.(Goal).

Mario Gavranovic
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uswisi, Mario Gavranovic, amerejea Dinamo Zagreb wiki chache tu baada ya kutoka klabuni hapo.
Nyota huyo aliona mkataba wake na klabu hiyo unamalizika msimu huu wa joto na alikuwa anajiandaa kuondoka, akiwa katika klabu hiyo ya Croatia tangu 2018.(Goal).

Adam Lallana
KLABU ya Brighton ipo mstari wa mbele kumsaini, Adam Lallana., reports the Times.
Kiungo huyo anajiandaa kuondoka Liverpool baada ya mechi ya jana dhidi ya Newcastle, akihitimisha miaka sita huko Anfield.
Lallana pia amekuwa akihusishwa na Leicester huku akijiandaa kwa uhamisho mwengine akiwa mchezaji huru.(Times).

Liberato Cacace.
KLABU ya Sint-Truiden ya Ublgiji wameweka mezani ofa kwa ajili ya nyota wa Wellington Phoenix, Liberato Cacace.
Kulingana na Stuff, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 anahitajika na klabu hiyo ya Ubelgiji, ambayo inasimamiwa na bosi wa zamani wa Melbourne Victory, Kevin Muscat.(Goal).

Thiago Alcantara
KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, ameeleza tena heshima yake kwa Thiago Alcantara, lakini, amekataa kuanika kwa kikosi chake kusaka saini ya kiungo huyo wa Bayern Munich.
Kiungo huyo amekuwa akitajwa kutaka kuondoka kwa mabingwa hao wa ‘Bundesliga’ (Goal).

Paul Arriola
KLABU ya D.C. United wameongeza mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kubakia kwa winga, Paul Arriola.
Mkataba wa Arriola ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2021, lakini, umeongezwa hadi mwisho wa kampeni ya 2024, idhini ya MLS inasubiri.(Washington Post).