Marc-Andre ter Stegen
CHELSEA imeweka mezani ofa kwa ajili ya mlinda mlango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen (28). (Cadena Ser).

Jadon Sancho
UHAMISHO unaokisiwa wa Jadon Sancho kwenda Manchester United uko karibuni kufikiwa, wakati Borussia Dortmund wakiwa tayari kukubali ada ya awali ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga huyo mwenye umri wa miaka 20. (Independent).

Raul Jimenez
MSHAMBULIAJI wa Mexico, Raul Jimenez (29), yuko njiani kuhamia Manchester United baada ya Wolves kukubali ada ya pauni milioni 27 kumsajili mshambuliaji wa Braga, Mreno Paulinho. (RTP).

David Alaba
CHELSEA na Manchester City ni miongoni mwa vigogo vinavyoongoza ambavyo vinafuatilia kama mchezaji David Alaba (28), atasaini mkataba mpya na Bayern Munich. (Telegraph).

Fabian Delph
KLABU ya Leeds inapanga kusajili wachezaji wawili, kiungo wa Everton Fabian Delph (30), na beki Danny Rose (30), wakati huu ambapo kocha, Marcelo Bielsa akitafuta wachezaji wenye uzoefu na Ligi Kuu ya England. (Star).

Sergio Romero
MLINDA mlango Muargentina, Sergio Romero (33), anataka kufanya mazungumzo na Manchester United kuhusu mustakabali wake huku Dean Hanserson (23), akirejea Old Trafford baada ya kukipiga kwa mkopo Sheffield United. (Sun).

Alexis Sanchez
KLABU ya Inter Milan inatarajiwa kukubali dili kumsajili mshambuliaji, Alexis Sanchez (31) kutoka Manchester United kwa mkataba wa kudumu msimu huu. (Manchester Evening News).

Pierre-Emile Hojbjerg
KLABU ya Southampton bado wanaisubiri Tottenham kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati, Pierre-Emile Hojbjerg (24). (Daily Echo).

Mesut Ozil
KIUNGO, Mesut Ozil (31) atasalia na Arsenal msimu huu. (Mail).

Lloyd Kelly
KLABU ya Liverpool inajiandaa kumsajili mchezaji wa Bournemouth, Lloyd Kelly (21), baada ya kupoteza fursa hiyo miezi 12 iliyopita alipokuwa akiichezea Bristol City. (Express).

Rhian Brewster
KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, atafanya uamuzi kuhusu mshambuliaji wa Kiingereza, Rhian Brewster (20), baada ya mchakato wa kucheza kwa mkopo Swansea kufanikiwa. (Liverpool Echo).