David Alaba
MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola, anatafakari uwezekano wa kumsajili beki wa kushoto wa Bayern Munich na Austria David Alaba (28), msimu huu wa joto. (Mirror).

Kevin de Bruyne
WAKALA wa Kevin de Bruyne amesema kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 29, hataondoka Manchester City, msimu huu hata marufuku ya Ulaya dhidi ya klabu hiyo itaondolewa. (Sporza).

Emiliano Martinez
ARSENAL inataka kusalia na kipa wa Argentina, Emiliano Martinez (27), baada ya kuahirisha mpango wa kumnunua kipa mpya msimu huu wa joto. (Mirror).

Luka Jovic
REAL Madrid wapo tayari kupokea ofa ya klabu zinazotaka kumnunua mshambuliaji wa Serbia, Luka Jovic (22). (Marca).

Jadon Sancho
MKURUGENZI wa michezo wa Borussia Dortmund, Michael Zorc, amesema, klabu hiyo ya Ujerumani imetoa orodha ya wachezaji watakaojaza pengo litakaloachwa na winga wa England, Jadon Sancho (20), endapo ataondoka msimu huo. (Kicker).

Ole Gunnar Solskjaer
MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameifahamisha klabu yake kwamba anataka kumsajili mshambuliaji atakayesaidiana na Sancho ambaye wanamnyatia pamoja na mshambuliaji wa kati na nyuma msimu huu. (Telegraph).

Olivier Giroud
INETR Milan inataka kumsajili beki wa kushoto wa Italia, Emerson Palmieri (25), na mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud (33), kutoka Chelsea. (Goal).

Hugo Lloris
KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Roy Keane ameshindwa kuchagua ni nani anastahili kujiunga na klabu hiyo kati ya kipa wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris (33), na mshambuliaji wa Korea Kusini, Son Heung-min (28). (Star).

Gabriel Magalhaes
EVERTON inakabiliwa na kibarua kigumu kumpata mlinzi wa Lille na Brazil, Gabriel Magalhaes (22), baada ya kuchelewa kuwasilisha ombi la kutaka kumnunu mchezaji huyo. (Sky Sports).

Jack Grealish
WAKALA wa mchezaji wa Aston Villa, Jack Grealish (24), amesema, kiungo huyo hajafikia makubaliano ya kujiunga na Manchester United huku klabu hiyo ikimuwekea thamani ya pauni milioni 80. (Metro).

Ben Godfrey
KLABU ya Norwich City imeitisha dau la pauni milioni 50 ili kumuuza beki, Ben Godfrey (22), huku klabu za Borussia Dortmund na RB Leipzig zikiwa miongoni mwa zinazomwania mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21. (Sky Sports).