JADON SANCHO
BORUSSIA DORTMUND haitakubali kitta cha chini ya euros milioni 130 pauni milioni 116 kwa winga wa England Jadon Sancho, 20, ambaye anaripotiwa kutakiwa na Manchester United. (Westdeutsche Allgemeine Zeitung, via Manchester Evening News)
KALIDOU KOULIBALY
BEKI wa kati wa Senegal Kalidou Koulibaly, 29, amesema anamaliza mkataba wake na Napoli, licha ya kudaiwa kutakiwa na Liverpool, Manchester City, Manchester United na Real Madrid. (La Gazzetta dello Sport – in Italian)
NEYMAR
BARCELONA inajaribu kusaka saini ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 28, kurudi tena Nou Camp msimu huu . (Marca)
LUKA JOVIC
LEICESTER inataka kumsaini mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 22, kutoka Real Madrid kwa pauni milioni 31 kuungana na shwahiba wake Jamie Vardy msimu ujao. (Mail on Sunday)
STEVEN GERRARD
TIMU ya daraja la ya Bristol City inamtaka bosi wa Rangers Steven Gerrard kuchukua nafasi ya kocha aliyefukuzwa Lee Johnson. (Sunday Express)
THIAGO ALCANTARA,
JUVENTUS na Manchester City zimeungana na Liverpool katika harakati za kumsaini kiungo wa Bayern Munich na Hispania Thiago Alcantara, 29. (Tuttomercatoweb – in Italian)
JONATHAN IKONE
CHELSEA na Inter Milan zimeanza mazungumzo na Lille juu ya uwezekano wa kumsajili mshambuliaji kutoka Ufaransa Jonathan Ikone, 22. (Le 10 Sport – in French)
JAMES RODRIGUEZ
BOSI wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hana uhakika kama kiungo mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 28, ataendelea kubaki klabuni hapo. (AS)
NICOLO ZANIOLO
JUVENTUS na Inter Milan zote zinamtaka kiungo mshambuliaji wa Roma na Itali Nicolo Zaniolo, 21,msimu huu. (Tuttosport – in Italian)