N’golo Kante
INTER Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N’Golo Kante huku Chelsea wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29. (Gazzetta dello Sport).

Kylian Mbappe
REAL Madrid inaamini mshambuliaji, Kylian Mbappe (21), atakuwa na mazungumzo nao kuhusu uhamisho kutoka Paris St-Germain. (Marca).

Dejan Lovren
LIVERPOOL ina mpango wa kumuuza beki wake, Dejan Lovren (31), ingawa anatafuta kuongeza mkataba wake. (Goal).

Kai Havertz
KAI Havertz (21), anataka kuondoka Bayer Leverkusen kwa sababu walishindwa kufuzu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo, Chelsea watalazimika kuhakikisha wanafuzu katika michuano hiyo ili kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumain kujiunga na timu hiyo. (Bild).

Tanguy Ndombele
BAYERN Munich wanajiandaa kuanza mchakato wa kumnasa kiungo wa Tottenham, Tanguy Ndombele (23), na Mfaransa mwenzie anayecheza nafasi ya kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko (25). (Le 10 Sport).

Rony Lopes
NICE imetoa ofa kwa kiungo wa Hispania, Rony Lopes anayekipiga Sevilla. (RMC Sport).

Stuart Webber
MKURUGENZI wa michezo wa Norwich, Stuart Webber amesema kwamba ombi la kutaka kumnunua mchezaji kinda mwenye kipaji mwisho wa msimu litaanza kwa dau la pauni milioni 20. (Norwich Evening News).

Ronan Curtis
KLABU ya Brentford inamlenga winga wa Portsmouth, Ronan Curtis (24) kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Said Benrahma ikiwa ataondoka kwenye klabu hiyo. (The News, Portsmouth).

Neymar
RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amekataa uwezekano wa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar (28), kurejea Nou Camp, lakini, amesema klabu inafikiria uhamisho wa mshambuliajji wa Inter Milan raia wa Argentina, Laitaro Martinez (22). (TV3 Mundo Deportivo).

Pep Guardiola
MANCHESTER City itatoa ofa ya mkataba wa muda muda mrefu kwa kocha, Pep Guardiola, baada ya marufuku dhidi ya klabu hiyo kufutwa.
Guardiola atapatiwa karibu kitita cha pauni milioni 150 kwa ajili ya kukipa nguvu kikosi cha ManCity. (Guradian).

Luca Jovic
AC Milan wanafikiria kumnunua mashambuliaji wa Real Madrid raia wa Serbia, Luca Jovic (22), ambaye anayekodolewa macho na Leicester City na Arsenal. (Calciomercato).