Amadou Diawara
KOCHA wa Leicester City, Brendan Rodgers anamfuatilia kwa karibu mchezaji wa Roma, Amadou Diawara. Kiungo huyo wa kati aliyetimiza miaka 23 jana, pia amehusishwa na Tottenham na Newcastle. (Leicester Mercury).

Paul Pogba
KIUNGO wa Ufaransa, Paul Pogba (27), yuko karibu kukubali mkataba mpya wa miaka mitano kuichezea Manchester United. (Sun).

Nicolas Tagliafico
BEKI wa kushoto wa Ajax, Nicolas Tagliafico (27), ni mchezaji muhimu kwa Manchester City msimu huu. (Sports Illustrated).

Thiago Alcantara
KIUNGO wa Hispania, Thiago Alcantara (29), anaamini, ataelekea Liverpool baada ya kukataa mkataba mpya na Bayern Munich.( Daily Mirror).

Malang Sarr
ARSENAL iko mbioni kumsajili beki Mfaransa, Malang Sarr (21), lakini, mchezaji huyo anayepatikana kwa uhamisho wa bila ya malipo akitokea Nice tayari ameshafuatiliwa na klabu za Italia na Ujerumani.( Sun).

Alvaro Fernandez
MANCHESTER United imekubali kuingia mkataba na beki wa kushoto wa Real Madrid, Alvaro Fernandez Carreras (17), ambaye atatia saini mkataba wa miaka minne kukipiga Old Trafford. (AS).

Mauricio Pochettino
KOCHA wa zamani wa Southampton na Tottenham, Mauricio Pochettino yuko kwenye orodha ya Inter Milan na Juventus ikiwa klabu hizo za Italia zitawafuta kazi makocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte na Maurizio Sarri mwishoni mwa msimu. (Daily Telegraph).

Jude Bellingham
KIUNGO wa kati Muingereza, Jude Bellingham (17), amekamilisha vipimo vya matibabu katika klabu ya Borussia Dortmund kabla ya kuondoka Birmingham, lakini, kwanza atakamilisha msimu huu na ‘The Blues’ (Sky Sports).

Serge Aurier
TOTTENHAM inaweza kumkosa mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Serge Aurier (27), baada ya kurudi Ufaransa kutokana na kifo cha kaka yake. (Evening Standard).

Allan
EVERTON imetoa ofa kwa kiungo wa Napoli, Allan, lakini, klabu hiyo ya Italia imesitisha makubaliano na mchezaji huyo Mbrazili mwenye umri wa miaka 29. (Sport Witness).

Ferran Torres
MANCHESTER City imekubaliana na masharti ya winga wa Valencia, Muhispania Ferran Torres (20). (Eurosport).