JOHN MCGINN

KOCHA wa Newcastle Steve Bruce anapanga uhamisho wa kiungo wa kati John McGinn, 25, raia wa Scotland ikiwa Aston Villa itashushwa daraja. (Star)

TODD CANTWELL

LEICESTER na Newcastle wameingia kwenye orodha ya timu zenye kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Norwich Todd Cantwell. (Mail)

NICOLAS TAGLIAFICO

CHELSEA na Atletico Madrid zinafuatilia beki wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 27, ambaye amehusishwa na kuhamia Manchester City. (Sun)

RALPH HASENHUTTL

KOCHA wa Southampton Ralph Hasenhuttl ameiambia Tottenham itoe ofa nzuri kwa kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, baada ya Everton kufungua uwanja wa kumwania mchezaji huyo kwa kitita cha karibu pauni milioni 25. (Evening Standard)

JOSE MOURINHO

KOCHA wa Tottenham Jose Mourinho anaamini kwamba kiungo wa kati wa Uingereza Oliver Skipp, 19, ambaye amesaini makubaliano mapya na klabu hiyo, ndio nahodha wa siku zijazo wa Spurs. Skipp anataka kuondoka kwa mkopo kupata ujuzi lakini Mourinho anapendelea mchezaji huyo asalie. (Evening Standard)

ALFIE DEVINE

TOTTENHAM iko tayari kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Wigan Alfie Devine, 15. (Mail)

FERRAN TORRES

MANCHESTER CITY imejitolea kwa kila namna kumsajili winga wa Valencia Ferran Torres, 20, lakini imeiarifu klabu ya Uhispania kwamba haitalipa zaidi ya euro milioni 35 sawa na (£31.8m) kwa mchezaji huyo. (Marca)

IKER CASILLAS

ALIYEKUWA mlinda lango wa Uhispania Iker Casillas, 39, anarejea Real Madrid kama mshauri, miaka mitano baada ya kuondoka na kujiunga na Porto. (Marca)

TIMOTHY FOSU-MENSAH

MANCHESTER UNITED itampa fursa mchezaji wa Uholanzi Timothy Fosu-Mensah, 22, ya kutafuta hatma yake ya kudumu katika klabu hiyo huku klabu nyingine za Ujerumani zikijitokeza kuonesha nia ya kumuwinda (Manchester Evening News)