MASON GREENWOOD
MSHAMBULIAJI Manchester United Mason Greenwood kutoka Uingereza, 18 atakuwa na mpango mpya wenye thamani ya pauni 40,000 kwa wiki – miezi tisa tu baada ya kusaini mkapab mpya. (Sun on Sunday)
JOHN TERRY
KOCHA Msaidizi wa Aston Villa John Terry anafikiriwa na Bristol City kuwa meneja wao mpya baada ya chaguo la kwanza Steven Gerrard kukataa kujiunga nao (Sunday Express)
JOELSON FERNANDES
ARSENAL wako tayari kutoa kitita cha pauni milioni 40 kwa mshambuliaji kutoka Lisbon Ureno U- 17 Joelson Fernandes, ambaye pia Barcelona na Juventus zote zinavutiwa na mchezaji huyo. (A Bola – in Portuguese)
CHRIS WILDER
BOSI wa Sheffield United Chris Wilder amesema kusajiliwa kipa Wes Foderingham, 29, haina maana kuwa Dean Henderson ataondoka klabuni hapo nabado ana matumaini ya kubakia ambaye abnacheza kwa mkopo kutoka Manchester United kwa msimu mwengine. (Mail on Sunday)
HENDERSON
CHELSEA bado hawajaamua kuendelea kubaki aua kaucahana na Henderson. (Sunday Express)
ANGUS KINNEAR
MTENDAJI mkuu wa Leeds Angus Kinnear anasema wamiliki wa klabu hiyo watakutana na meneja Marcelo Bielsa wiki ijayo, kujadili mkataba mpya na kufanya kazi kwa lengo la kujua masauala ya uhamisho, kwenye ligi kuu msimu ujao. (Sunday Express)
DEJAN LOVREN,
ZENIT ST PETERSBURG wako tayari kutoa karibu pauni milioni 9 kwa mlinzi wa Liverpool Dejan Lovren, 31, lakini mabingwa hao wa Uingereza wanaweza kudai karibu pauni milioni 15 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia.(Mail on Sunday)
SANTI CAZORLA
VILLARREAL ilithibitisha Santi Cazorla amekataa kuongeza chagua kutokuongeza mkataba wake na klabu hiyo, huku kukiwa na uvumi wa kiungo wa Uhispania, 35, angeweza kurudi Arsenal kufundisha. (Sunday Mirror)
JADON SANCHO
BORUSSIA DORTMUND wameweka kitita cha bei ya pauni milioni 115 kwa Jadon Sancho, 20, lakini mchezaji huyo wa England, anayehusishwa kujiunga na Manchester United, amekataa kuondoka katika klabuni hiyo ya Ujerumani.
(Sunday Express)