Achraf Hakimi
MENEJA wa Real Madrid, Zinedine Zidane alichangia kwa mchezaji wa Morocco, Achraf Hakimi (21), kuondoka katika klabu hiyo ya Hispania ili kujiunga na Inter Milan, kulingana na wakala wa beki huyo. (Marca).
Declan Rice
MENEJA wa Chelsea, Frank Lampard, amemlenga kiungo wa kati wa West Ham na England, Declan Rice (21), kama chaguo muhimu kwa kikosi chake.(Times).
Kalidou Koulibaly
MANCHESTER City na Manchester United zinawanyatia mabeki wawili tofauti huku beki wa Napoli na Senegal, Kalidou Koulibaly (29), na beki mwenye umri wa miaka 25, Milan Skriniar, anayeichezea Inter Milan na Sloviakia, wakilengwa . (Independent).
Sergej Milinkovic
KLABU za Chelsea na Real Madrid zimeimarisha juhudi za kumsaini kiungo wa kati wa Lazio, Sergej Milinkovic – Savic huku wakijaribu kuwa kifua mbele kuzipiku Manchester United na PSG kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Serbia. (Gazzetta dello Sport).
Nathan Ake
MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer alimwambia beki wa kati wa Bournemouth, Nathan Ake kwamba wanahitaji beki wa mguu wa kushoto, hivyo, endelea kuimarika baada ya kukamilika kwa mechi ambayo Bournemouth iliteza 5-2 katika uwanja wa Old Trafford. (Telegraph).
Odsonne Edouard
CRYSTAL Palace inapanga uhamisho wa dau la pauni milioni 25 kumnunua mshambuliaji wa Celtic na Ufaransa, Odsonne Edouard (22). (Sun).
David Alaba
BAYERN Munich itamuachia beki wa Austria, David Alaba (28), ambaye kandarasi yake inakamilika 2021, kuamua iwapo anataka kusalia na klabu hiyo ama kuhamia katika Ligi Kuu ya England. (Mirror).
Dayot Upamecano
RB Leipzig inatarajia kwamba beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21, Dayot Upamecano, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Arsenal , ataongeza kandarasi yake baada ya kukamilika 2021. (Mirror).
Jorginho
KLABU ya Juventus inataka kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea na Italia, Jorginho (28) mwisho wa msimu huu. (Tuttosport).
Gareth Bale
REAL Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji yeyote mwisho wa msimu huu kutokana na athari za mripuko wa corona. Badala yake , inatumai itachangisha pauni milioni 190 kupitia uuzaji wa wachezaji huku winga Gareth Bale (30), akihusishwa na uhamisho. (Marca).
John Terry
BEKI wa zamani wa England, John Terry, ambaye ni naibu wa kocha wa Aston Villa, Dean Smith, anatarajiwa kuwa meneja mpya wa klabu ya ligi ya daraja la kwanza, Bristol City. (Football Insider).