Antoine Griezmann
KUSOTA kwa mshambuliaji wa Barcelona, Antoine Griezmann, klabuni hapo kunaweza kuipa nafasi Arsenal au Inter Milan kumsaini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29. (Express).
Thiago Silva
KLABU ya Arsenal inaamini beki wa kati, David Luiz (33), anaweza kumshawishi Mbrazil mwenzake, Thiago Silva (35), kujiunga na klabu hiyo baada ya kuondoka Paris St-Germain majira haya ya kiangazi. (Le10 Sport).
Thomas Partey
ARSEBAL wameongeza shauku yao kwa kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey, lakini, hawataki kukutana na kifungu chake cha pauni milioni 45. (Athletic).
Serge Aurier
BEKI wa Tottenham na Ivory Coast, Serge Aurier (27), anaivutia klabu ya ‘Ligue 1’ ya Monaco ambapo inatarajia kumsaini mchezaji huyo msimu huu wa joto. (Sky Sports).
Andreas Christensen
BEKI wa kimataifa wa Chelsea raia wa Denmark,Andreas Christensen (24), amesema hana papara ya kuondoka klabuni hapo na yupo wazi kusaini mkataba mpya Stamford Bridge. (Goal.com).
Henrikh Mkhitaryan
KIUNGO wa Arsenal na Armenia, Henrikh Mkhitaryan (31), anajiandaa kusaini mkataba wa kudumu na Roma baada ya mkataba wake wa mkopo na miamba hiyo ya ‘Serie A’. Lakini, winga wa Uholanzi, Justin Kluivert (21), hatarajiwi kwenda sehemu nyengine.(Mail).
Quique Setien
BOSI wa Barcelona, Quique Setien anaingia chini ya shinikizo kubwa na meneja wa Uholanzi, Ronald Koeman, ambaye amesema alipuuza nafasi ya kuinoa klabu hiyo ya Nou Camp mnamo Januari, alionekana akiingia katika sehemu mpya jijini hapo. (Mail).
Mohamed Salah
WINGA wa Liverpool na Misri, Mohamed Salah (28), amesema, anataka kubakia na klabu hiyo kwa muda mrefu. (Bein Sports).
Largie Ramazani
YOSO wa Manchester United, Largie Ramazani (19), anakaribia kutimkia klabu ya daraja la pili la Hispania ya Almeria. Raia huyo wa Ubelgiji alikataa ofa ya kubakia Old Trafford. (Manchester Evening News).
Eduardo Camavinga
MKURUGENZI wa michezo wa Rennes, Florian Maurice, amesema klabu hiyo ya ‘Ligue 1’ hauna nia ya kumuuza kiungo wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21, Eduardo Camavinga huku akitolea nje Real Madrid, hata kwa euro milioni 80.(AS).