Achraf Hakimi
BEKI wa Real Madrid, Achraf Hakimi (21), ameonekana Italia kabla ya uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Inter Milan. (Mail).

Jadon Sancho
MANCHESTER United haitalipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa winga wa Borussia Dortmund ,Jadon Sancho.
Hata hivyo, klabu hiyo ya Bundesliga inataka ongezeko la pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports).

Matteo Guendouzi
ARSENAL wanafikiria kumtumia kiungo wa kati, Matteo Guendouzi (21), kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu. (Mail).

Pierre-Emile Hojbjerg
TOTTENHAM wanaamini watampata kiungo wa Southampton, Pierre-Emile Hojbjerg (24), msimu huu, lakini, watapaswa kuuza wachezaji kwanza. (Telegraph).

Nathan Ake
MANCHESTER City wana mpango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Bournemouth, Nathan Ake (25). Hata hivyo wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Chelsea ambayo pia wanamtaka mchezaji huyo. (Athletic).

Marc Jurado
BEKI wa kulia wa Barcelona, Marc Jurado (16), ameondoka katika klabu hiyo ya Catalan. Muhispania huyo anajiandaa kujiunga na Manchester United msimu huu.(ESPN).

Ferran Torres
JUVENTUS imeongeza ushawishi wao kwa winga Muhispania anayeichezea Valencia, Ferran Torres (20). Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na kuhamia Manchester United na Borussia Dortmund. ( Mail via Onda Cero).

Leroy Sane
MANCHESTER City imekubali kumuuza winga, Leroy Sane kwa Bayern Munich, mchakato utakaowaingizia kiasi cha pauni milioni 54.(Mail).

Pablo Moreno
MANCHESTER City imekamilisha mkataba wa kubadilishana wachezaji ambao utamuwezesha mshambuliaji, raia wa Hispania Pablo Moreno (18) kujiunga nao kutoka Juventus, huku winga Mreno, Felix Correia (19), akielekea upande wa ‘Serie A. (Guardian).

Layvin Kurzawa
MCHEZAJI anayelengwa na Arsenal, Layvin Kurzawa (27), anatarajiwa kutia saini mkataba mpya wa miaka minne na Paris St-Germain wakati kandarasi ya beki huyo wa kushoto wa Ufaransa itakapokamilika Juni 30.(RMC Sport).

Henrikh Mkhitaryan
AS Roma imethibitisha kuwa mkopo wa Henrikh Mkhitaryan kutoka Arsenal umeongezwa mpaka mwishoni mwa msimu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alijiunga na timu hiyo ya Serie A mwezi Septemba. (Evening Standard).