Dean Henderson
CHELSEA imejitayarisha kutoa ofa ya pauni 170,000 kwa wiki kwa ajili ya mlinda mlango Muingereza, Dean Henderson (23), ambaye sasa hivi yuko Sheffield United kwa mkopo, kujaribu kumshawishi kujiunga nao akitokea Manchester United. (Manchester Evening News).

David de Gea
MLINDA mlango, Dean Henderson atatafuta kwa kila namna kuondoka tena kwa mkopo labda tu apate hakikisho kutoka Manchester United kwamba atapata fursa ya kushindana na mlinda mlango wa Hispania, David de Gea (29), awe chaguo la kwanza. (Times).

Marc-Andre ter Stegen
KLABU ya Chelsea pia itajitahidi kusaini mkataba na mlinda mlango wa Barcelona na Ujerumani, Marc-Andre ter Stegen (28), na ipo tayari kutoa ofa kwa nyanda wa kimataifa, Kepa Arrizabalaga (25), kama sehemu ya makubaliano yoyote. (Mundo Deportivo).

Mikel Arteta
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta ana uhakika kwamba mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang (31), atasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Independent).

Pierre-Emile Hojbjerg
KLABU ya Everton ina nia ya kumsajili kiungo raia wa Denmark anayekipiga Southampton, Pierre-Emile Hojbjerg (24), lakini amewaarifu kwamba angependelea zaidi kujiunga na Tottenham. (Liverpool Echo).

Alphonse Areola
MLINDA mlango wa Paris St-Germain, Alphonse Areola (27), ambaye yuko kwa mkopo Real Madrid, huenda akawa njiani kwenda klabu za Uingereza baada ya mchezaji huyo raia wa Ufaransa kununua nyumba ya familia yake mjini London. (Marca).

Steve Bruce
KOCHA wa Newcastle United, Steve Bruce, ataendelea na kazi yake ikiwa Henry Mauriss, mpinzani wa Saudi Arabia ambayo pia anataka kuinunua klabu hiyo, atainunua ‘Magpies’. (Telegraph).

Andrea Radrizzani
MMILIKI wa Leeds United, Andrea Radrizzani, amesema, ataangalia kumleta mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani (33), katika klabu hiyo baada ya kupandishwa Ligi Kuu ya England. Cavani aliondoka Paris St-Germain msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika. (Sky Sports Italia).

Valentino Lazaro
WINGA raia wa Austria wa Newcastle United ambaye yuko kwa mkopo, Valentino Lazaro (24), anafikiria mara mbili kuhusu kuondoka Inter Milan kwa sababu ya kutopangwa kushiriki kweye mechi na St James’ Park. (Chronicle).

Thomas Soucek
KLABU ya West Ham itahitajika kubadilisha mkataba wa mkopo wa kiungo raia wa Jamhuri ya Czech, Tomas Soucek (25), kutoka Slavia Prague hadi kuwa wa kudumu kwa pauni milioni 18.9, baada ya kuthibitishwa kwamba itaendelea kushiriki kwenye Ligi Kuu ya England.(Telegraph).