TURIN, Italia
JUVENTUS wamepoteza nafasi ya kubeba taji la ‘Serie A’ huku bosi Maurizio Sarri akishangaa kipigo walichokipata mbele ya Udinese, wakilala magoli 2-1.

Juve ambayo wamekuwa mabingwa wa Italia kwa siku 3,000, wanahitaji kushinda mchezo wao mmoja wa mwisho ili kushinda taji la tisa mfululizo.

Walifanikiwa kuongoza kwa goli lililofungwa na Matthijs de Ligt kabla ya Ilija Nestorovski kusawazisha kwa kichwa safi huku Seko Fofana, akifunga goli la ushindi dakika za mwishoni.
“Tumelipia ukosefu wa utaratibu baada ya nusu nzuri ya kwanza,” alisema, Sarri, ambaye hatma yake inaripotiwa kuwa na shaka.

“Tulitaka kushinda kwa gharama zote, tulikuwa fujo na tulichukua mchezo huo kwa njia ya hatari na tukapoteza kwenye dakika 93 kwa sababu tulitaka pointi hizo tatu.

“Katika hatua hii ya msimu, ni ngumu, sote tumechoka. tumepoteza hasira.
“Ni ngumu kukaa kiakili na kiwiliwili kwenye mpira kwa dakika 90. Michezo ni ya kushangaza na kasi hubadilika kwa urahisi sana. Uchovu wa akili ni zaidi ya uchovu wa mwili.”
Cristiano Ronaldo amepitwa na mshambuliaji wa Lazio, Ciro Immobile kwenye mbio za kiatu cha dhahabu. Immobile alifunga bao lake la 31 la msimu huu katika ushindi wa 2-1 wa Lazio dhidi ya Cagliari lililomchukua moja juu ya Ronaldo.

Juventus walihitaji pointi tatu tu ili kutwaa taji la ‘Serie A’ kwa msimu wa tisa mfululizo, lakini, walikuwa nje ya kiwango.

Wameshinda moja tu ya michezo yao mitano ya ‘Serie A’ iliyopita, lakini, timu tatu zilizo chini yao, Atalanta, Inter Milan na Lazio zote ziliangusha pointi hivi karibuni.

Sarri anatarajia kushinda taji la kwanza la ligi kwenye taaluma yake. Juve iliangalia kibarua kwa Udinese ambayo bado hajawa salama kutoka hatari ya kushuka daraja na mashuti yao 21 yalikosa kuziona nyavu.Watakipiga na na Sampdoria, ingawa wanaweza kutangazwa mabingwa kabla ya hapo ikiwa wapinzani wao watapoteza mechi zao za mwishoni mwa wiki.(AFP).