KAMPALA,UGANDA
WIZARA ya Afya
ya Uganda imetangaza kifo cha kwanza cha Covid-19 nchini ikiwa kesi
zilizothibitishwa ziliongezeka hadi kufikia 1,079.
Mkurugenzi mkuu wa huduma za afya Dkt Henry Mwebesa
alisema aliyefariki ni mfanyakazi wa Wilaya ya Namisindwa, mwenye umri wa miaka
34 raia wa Uganda.
Marehemu huyo alipokelewa Hospitali akiwa na dalili za Covid-19 na kutengwa katika wodi maalumu baada ya hali yake kuwa mbaya na hatimae kuzikwa kwa taratibu za Kiserikali.
Uchunguzi zaidi uligundua kuwa alikuwa raia wa Uganda
kutoka Manafwa, Bubulo Mashariki, Namabya Namunyali Sisongofwa, “Dk
Mwebesa aliwaambia waandishi wa habari jijini Kampala.
Mawasiliano ya marehemu huyo yatafuatiliwa kila siku kwa siku 14 ili kujua
watu wa karibu waliokuwa na marehemu kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa watu
wengine.
Jumla ya Waganda 971 wamepona virusi hivyo tangu kesi ya kwanza ilipothibitishwa Machi mwaka huu.