KAMPALA,UGANDA

WAZIRI  wa Afya wa Uganda Ruth Aceng ameweka maabara mbili zinazohamishika katika hatua ya kuongeza kasi ya upimaji wa COVID-19 hasa kwa madereva wa malori ya mizigo wanaovuka mipaka.

Aceng alisema maabara hizo zilizochangiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC zitasaidia watu kupimwa mahali popote walipo ili kutoa majibu salama,sahihi na kwa wakati.

EAC chini ya mradi wa Maabara zinazohamishika ilichangia maabara tisa kwa nchi zake wanachama, kwa lengo la kugundua na kuitikia COVID-19 pamoja na magonjwa ya mripuko kama vile Ebola.

Hadi sasa Uganda ina watu 1,000 walioambukizwa virusi vya corona, kati yao 908 walipona na hakuna kifo kilichoripotiwa.