BERLIN,UJERUMANI
SHERIA mpya kwa ajili ya upimaji wa lazima wa virusi vya corona kwa wasafiri wanaoingia Ujerumani kutoka nchi ambazo zinatajwa kuwa ni maeneo hatari itaanza kutumika wiki ijayo.
Hayo yalisemwa na msemaji wa wizara ya afya ya nchi hiyo jana katika mkutano wa kila siku na waandishi habari.
Ujerumani ilitangaza mipango siku ya Jumatatu kwa upimaji huru, wa lazima wa virusi vya corona kwa watu wanaorejea kutoka likizo mapumzikoni kutoka katika mataifa yanayoonekana kuwa katika hatari zaidi ili kupunguza kusambaa kwa maambukizi wakati msimu wa likizo za mapumziko ukianza.