NA ABOUD MAHMOUD

UMOJA wa Maaskari Wastaafu Zanzibar (UMAWA) Umempongeza, Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kupeperusha bendera ya Chama cha Mpainduzi (CCM) kuwania nafasi ya Urais kwa kuchaguliwa kidemokrasia na Mkutano mkuu wa chama kwa asilimia 78.68.

Katika salamu hizo za pongezi zilizotolewa na umoja huo zimesema kwamba wana imani kubwa na mgombea huyo kutokana na uzoefu wake wa uongozi katika Wizara ya Ulinzi pamoja na Wizara ya Afya.

“Tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kuchaguliwa kidemokrasia na Mkutano Mkuu wa CCM dhidi ya wagombea wengine, tuna imani kubwa na yeye kuiletea mafaniko Zanzibar kutokana na utendaji wake kutokana na nyadhifa mbali mbali alizowahi kuzishika,”.

UMAWA wamesema mbali na nafasi hizo kubwa katika Serikali lakini pia kutokana na taaluma yake ya udaktari utadumisha ulinzi na usalama wa nchi, ustawi wa jamiii pamoja na kuzidi kuinua uchumi wa nchi na kuimarisha Muungano wa Tanzania.

Aidha umoja huo ulieleza kwamba Dkt Hussein akiwa kijana wa mwana Mapinduzi wana hakika atadumisha Mapinduzi ya Zanzibar na kuinua hali ya maisha ya wananchi wote wa Zanzibar.

“Tuna imani kubwa na kijana wetu huyu wa mwana Mapinduzi kwamba ataweza kudumisha Muungano wetu wa Tanzania, Mapinduzi matukufu ya Zanzibar pamoja na kuinua uchumi”, ulisema umoja huo.

UMAWA umeahidi kumuunga mkono kwa asilimia 100 kiongozi huyo mtarajiwa na kumtakia kila la heri pamoja na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu