MADRID, Hispania
KOCHA wa zamani wa Arsenal, Unai Emery, ametangaza rasmi kurejea kufundisha soka nchini Hispania, akiinoa Villarreal.

Emery (48), anajiunga na Villarreal kama mrithi wa kocha, Javi Calleja aliyeoondoka licha ya kumaliza msimu akiiacha Villarreal nafasi ya tano katika msimamo wa ‘La Liga’ na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Europa msimu ujao.

Hii ni mara ya kwanza Unai anarudi kufundisha timu tokea alipofukuzwa na Arsenal mwezi Novemba 2019 baada ya kudumu kwa miezi 18 pekee, akiwa kajiunga nao Mei 2018 kurithi mikoba ya Arsene Wenger.
Unai amewahi kufundisha kwa mafanikio klabu za PSG, Sevilla na Valencia.(Goal).