BRASILIA,BRAZIL
UTAFITI mpya uliochapishwa nchini Brazil, unaonesha matumizi ya dawa aina ya hydroxychloroquine katika kukabiliana na kitisho cha janga la COVID-19 hayana matokeo yoyote.
Hatua hiyo inatajwa kuwa ni pigo jengine kwa Rais Jair Bolsonaro ambaye amekuwa akitoa msukumo mkubwa katika matumizi yake.
Kumefanyika majaribio katika hospitali 55 katika maeneo tofauti ya Brazil ambayo yalionesha kuwa dawa hiyo haina uwezo wowote katika kuwasaidia wagonjwa.
Kama ilivyokuwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, Bolsonaro amekuwa akiwashikiza watu kuitumia kama tiba ya ugonjwa wa COVID-19.
Brazil kwa wakati huu inashika nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya maambukizi na vifo vinavyotokana na janga hilo,baada ya Marekani ikiwa na maambukizi milioni 2.3 na vifo 84,000.
Bolsonaro, ambaye anavipuuza virusi hivyo kama mafua madogo,anakosoa vikali athari za kiuchumi zinazotokana na hatua za kujitenga kwa jamii, akisema ni mbaya zaidi kuliko ugonjwa wenyewe.