PARIS, UFARANSA

RIPOTI  ya kimataifa imeonyesha kuwa njaa, utapiamlo na uzito uliopitiliza sio tu vinasababisha tatizo la kiafya katika nchi zinazoendelea,bali pia linachangia matatizo ya kiuchumi ambayo huzigharimu kampuni hadi dola bilioni 850 kwa mwaka.

Ripoti hiyo ilieleza  kuwa utapiamlo unasababisha hatari kama vile mripuko wa magonjwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kuchangia kupungua kwa uzalishaji na mapato.

Kiongozi wa watafiti wa ripoti hiyo,Laura Wellesley alisema kwenye nchi zinazoendelea ambako ongezeko la utapiamlo liko juu,wanakadiria kuwa gharama za kupungua kwa uzalishaji zitakuwa kati ya dola bilioni 130 na bilioni 850 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Lishe Ulimwenguni kwa mwaka 2020, takriban mtu mmoja kati ya watu tisa duniani ana njaa au ana utapiamlo, huku mtu mmoja kati ya watu watatu ana uzito uliopitiliza.