ANKARA,UTURUKI

ENEO la mashariki ya bahari ya Mediterania ambako meli ya Uturuki inafanya utafiti wa miamba chini ya bahari ni sehemu ya eneo la Uturuki, Ankara ambayo inapuuza shutuma za Ugiriki kuwa meli hiyo inaingilia eneo lake.

Hali ya wasi wasi ya muda mrefu kati ya washirika hao wa jumuiya ya NATO iliongezeka baada ya meli ya kijeshi ya Uturuki  kutoa tahadhari inayojulikana kama Navtext kwa ajili ya utafiti wa miamba katika eneo la maji kati ya Cyprus na Crete.

Ugiriki na Uturuki zinavutana kuhusiana na madai yanayokinzana kuhusiana na maliasili za mafuta na gesi , yaliyomulikwa zaidi kutokana na majaribio ya nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Cyprus pia inafanya uchunguzi wa gesi ya asili katika eneo hilo la mashariki mwa bahari ya Mediterania licha ya upinzani mkali kutoka Uturuki.