LONDON, England

JAMIE VARDY mshambuliaji anayekipiga ndani ya klabu ya Leicester City ni moto wa kuotea mbali kwa kucheka na nyavu ndani ya ligi kuu England.

Amefunga jumla ya mabao 23 na kutoa jumla ya pasi 5 zilizoleta mabao ndani ya timu hiyo.

Ametumia jumla ya dakika 2,944 ndani ya uwanja na ana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 128.

Anafuatiwa na Danny Ings wa Southampton mwenye jumla ya mabao 21 akiwa ametumia dakika 2,722 akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 130.