ABUJA,NIGER

VIONGOZI  wa Afrika Magharibi wameuhitimisha mkutano wao wa siku nzima nchini Mali bila mpango madhubuti wa kupunguza mgogoro wa kisiasa uliokuwa ukiongezeka.

Viongozi watano wa ukanda huo, walikutana na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita na kwa upande mwengine viongozi wa harakati za maandamano wanaoshinikiza ajiuzulu, katika kipindi hiki ambacho pia makundi ya wenye itikadi kali yanatishia taifa hilo kuliingiza katika vurugu.

Hata hivyo hatua ya viongozi hao kuingilia mzozo huo, haijazaa matunda yoyote na Rais wa Niger Mahamadou Issoufou sambamba na viongozi wa Senegal, Ivory Coast, Ghana na Nigeria walisema umoja wao wa ECOWAS utafanya mkutano wa kilele Jumatatu.