NAIROBI,KENYA

VISA  vya maambukizi ya Corona nchini kenya vimefikia watu 10,105 huku majimbo yaliopo mipakani yakishuhudia kupata virusi hivyo kutoka mataifa jirani.

Serikali ya kenya inasisitiza watu kutilia mkazo maagizo ya afya ili kuzuia maambukizi kusambaa katika jamii zinazoishi mipakani.

Kwa mujibu wa wizara ya afya Kenya majimbo matatu ikiwemo Kajiado, Busia na Kwale ingawa visa hivyo vinathibitishwa lakini bado kuna changamoto.

Kati ya mikakati kwenye mipaka hiyo ni kuhakikisha madereva wa malori ya mizigo na matrela wanapimwa kabla ya kuruhusiwa kuingia kenya.

Katika kaunti ya Kwale ambayo inaunganisha nchi ya kenya na Tanzania kwenye mpaka wa Lungalunga kati ya visa 139 ambavyo viliripotiwa tangu mwezi Marchi, visa 80 ni raia wa Tanzania na Malawi.

Haya yanajiri baada ya muafaka uliopatikana kati ya Kenya na Tanzania mapema mwezi Juni, wakati ambapo msongamano wa malori ulishuhudiwa mpakani huku kila nchi ikimnyooshea mwenzake kidole cha lawama.

Naye kaimu mkurugenzi wa afya kenya, Dr. Partric Amoth, alisema kuwa mikakati ya mipakani ilisaidia kudhibiti maambukizi kusambaa kwenda jamii zinazoishi karibu.

Alisema Serikali inatumia mabalozi wa nyumba kumi pamoja na raia katika kuwafichua raia wa Tanzania na wakenya wanaotumia njia za vichochoroni kuingia ndani ya taifa jengine.

Haya yanajiri huku Kenya ikiripoti visa 10,105 hadi sasa.