NA ASIA MWALIM

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye kufundisha jamii, zikiwemo sheria, ukuaji wa uchumi na maendeleo yanayo husu jamii.

Msaidizi Mkurugenzi wa Mipango na Utawala baraza la Manispaa wilaya ya Magharibi ‘B’ Ameir Ali Haji, Aliyasema hayo alipokua akizungumza na mwaandishi wa habari hizi, huko ofisini kwake Mchina Mwisho Unguja.

Alisema ikiwa waandishi wa habari watachukua jiitihada za kuelimisha jamii maendeleo ya kiafya, kiuchumi, na kisiasa yaliopatikana nchini, hatua hiyo itaweza kuleta mabadiliko na mafanikio makubwa kwa wananchi.

Alisema Serikali imechukua juhudi kubwa kuhakikisha inaimarisha miundo mbinu barabara, maji safi na salama, ujenzi wa Skuli pamoja na kujenga vituo vya afya maeneo ya mjini na vijiji.

Akizungumzia suala la uchumi, alisema nchi ya Tanzania imefika uchumi wa kati, hatua hiyo imepatikana kutokana na jitihada kubwa za Serikali kupambana, ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.  

Alieleza kuwa, wananchi wanapaswa kuyajua maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini, chini ya uongozi Mahiri wa Dk, Ali Mohamed Shein, katika kuteleza vyema ilani yake katika kipindi cha awamu ya saba.

Akizungumzia suala la biashara, aliwaataka Waandishi, kuandika habari zinazo husiana na sheria, ambazo wanalazimika kuzijua na kuzifata wafanyabiashara, hatua hiyo itapelekea kuleta mabadiliko nchini.

Alifahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia bunge lake tukufu imeweza kupanga na kupitisha sheria mbalimbali zinazohusu maendeleo ya biashara kwa wananchi wake ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika sekta zote nchini.

“Wafanya biashara wana sheria zao zilizowekwa na wanapaswa kuzifuata ili kuhakikisha wanaenda sawa na maelekezo yaliyotolewa na serekali” alisema.

Aidha alisema licha ya jitihada kubwa zinazo chukuliwa na serekali kuwahamasisha wafanyabiashara waweze kwenda sambamba na sheria zilizowekwa ikiwemo kukata leseni kwa muda husika, lakini wapo wanao dharau agizo hilo na kusahau kuwa wanaenda kinyume na agizo la serikali, jambo ambalo litarudisha nyuma maendeleo.

Aidha aliwataka wafanyabiasha kufuata sheria, na mikakati imara iliopangwa nchini, kufanya hivyo kutasaidia kuiboresha nchi kupata maendeleo zaidi.