NA LAYLAT KHALFAN

 WAFUGAJI nchini wameshauriwa kuhakikisha wanawanachanja wanyama wao kwa wakati ili kuwakinga na maradhi yanayojitokeza sambamba na kutumia mbinu za kisasa za ufugaji kwa lengo la kupata soko la uhakika.

Mkurugenzi wa Idara ya Maliasili Mifungo na Mazingira, Hassan Juma Salum, wa Baraza la Manispaa Magharibi ‘A’, alitoa ushauri huo ofisini kwake Kianga wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili.

Alisema mara nyingi wanyama wamekuwa wakishambuliwa na maradhi mbalimbali ikiwemo  ya ngozi ambayo yamekuwa yakiwaathiri zaidi wanyama ukilinganisha na maradhi mengine ya mripuko kama vile chambavu , bekota  ambayo yanakuwa ni mara chache kujitokeza.

“Tumekuwa tukiwahamasisha kuhusu masuala ya chanjo na baadhi ya chanjo tumefanikiwa kuzitoa bure bila malipo yoyote”, alisema.