MALLETTA, MALTA
KUNDI la wahamiaji 63 waliokolewa kutoka kwenye mashua yao iliyokuwa tayari imeshaanza kujaa maji baada ya kupigwa na mawimbi makali huko Malta wameokolewa na sasa wamewasili Malta, vyombo vya habari vya Times Times vya Malta viliripoti jana.
Wahamiaji hao waliokolewa mapema siku iliyofuatia baada ya kuwasiliana na shirika lisilo la kiserikali kuombwa msaada kwa njia ya simu.
Hatua hiyo ilikuja siku ya Alkhamis wakati mashua yao ilikuwa ikielekea kuzamz katika bahari ya Mediterania.
Msemaji wa Kikosi cha Wanajeshi wa Malta (AFM) alisema walilazimika kuwaokoa wahamiaji hao waliokuwa katika hatari ya kufa maji.