NAIROBI,KENYA
KARIBU watu milioni 3.6 nchini Kenya wako kwenye hatari ya kukumbwa na njaa wakati nchi inapambana na janga la Covid-19.
Wakenya walio hatarini wako kwenye dimbwi la zaidi ya bilioni moja, au asilimia 16 ya idadi ya watu ulimwenguni,ambao wanakabiliwa na shida ya muda mrefu ya kibinadamu.
Ripoti ya msaada wa Kibinadamu ulimwenguni 2020, iliyochapishwa na Shirika la Utafiti la Maendeleo la mipango ya Uingereza, inaorodhesha nchi nyingi kuingia katika janga hilo la njaa.
Kenya na Ethiopia ziliorodheshwa pamoja na Sudani Kusini,Libya, Somalia na Jamhuri ya Afrika ya Kati kama ni nchi zilizo na kiwango cha juu cha mahitaji.
Somalia nayo watu milioni 5.2 waliathiriwa na janga la corona, Zimbabwe watu milioni 5.1, Chad milioni 4.8,Mali milioni 3.9 na Kenya watu milioni 3.6.